WIZARA YA AFYA YAZUIYA LIKIZO KWA MADAKTARI NA WAUGUZI.
Na
Heri Shaaban
NAIBU WAZIRI wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt, Faustine
Ndugulile ameziagiza Halmashauri kuangalia upya utoaji wa likizo kwa Madaktari
na Wauguzi katika kipindi cha kufunga mwaka kutokana na idadi ya wagonjwa kuwa
kubwa .
Dkt .Ndungulile alisema hayo
Wilayani Ilala katika vituo vya afya alivyotembelea jimboni Segerea
ambavyo ni Buguruni Plani ,Tabata A na segerea Ugombolwa .
" Kipindi cha mwisho wa
mwaka kina changamoto kwa upande wa wagonjwa wanakuwa wengi, hivyo kabla ya
kuwapa rikizo taratibu za utoaji zifuatwe lengo wagonjwa waweze kupata huduma
kwa wakati" alisema Ndungulile.
Katika ziara yake ameweza kujionea idadi ya wagonjwa wengi wakisubiri matibabu katika vituo vya afya alivyotembelea katika ziara yake hiyo ya kikazi.
Aidha katika hatua nyingine Naibu Waziri Ndungulile amepiga marufuku wagonjwa kuandikiwa kununua dawa nje ya vituo vya afya vya serikali badala yake wagonjwa wote wapewe dawa katika vituo hivyo vya serikali kwani imenunua dawa za kutosha.
Aliwakikishia wananchi Wizara imeshasambaza dawa katika vituo vya afya nchi nzima lengo kuwapa huduma bora.
Wakati huohuo ametoa muda wa miezi mitatu Manispaa ya Ilala kuboresha mfumo wa Mapato na Maabara katika Hospitali ya Plani iliyopo Buguruni Mnyamani.
Kwa upande wake Mbunge wa Segerea (CCM) Bonah Kaluwa amemuomba Naibu Waziri kuongea na Serikaki Kuu ili kuarakisha Wakala wa Barabara TARURA kujenga Barabara ya Mnyamani ili wagonjwa wafike kwa wakati kupatiwa matibabu.
"Kilio changu barabara ya Mnyamani wananchi wangu wanapata shida njia mbovu muda mrefu mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa gari la wagonjwa pia linapita kwa shida kupeleka wagonjwa wa rufaa "alisema Kaluwa.
Pia aliomba Wizara kuipandisha hadhi zahanati hiyo ya Plani .
Naye Dkt. wa Zamu Msimamizi wa Vitendo Neema Ntabaye alisema madktari waliopo 12 wana kabiliana na changamoto ya jengo la upasuaji.



Comments
Post a Comment