RC MAKONDA AZIOMBA MAMLAKA KUSIMAMISHA MASOMO KWA MUDA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul
Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko.
Aidha na kuwataka wananchi waishio maeneo ya
mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao.
Amesema kuwa hadi sasa zaidi
ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo
ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari.
RC
Makonda amesema kufuatia mwendelezo wa mvua hizo ameziomba Mamlaka husika
kusimamisha masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na
Maafa.
Aidha RC Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo Madaraja, Barabara,Shule pamoja na kuzibua mitaro.
Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya Upanga RC Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina.
Pia amewasihi wakazi wa jengo hilo pamoja na majirani kutafuta sehemu ya kujisitiri kwa wakati huu kwa mustakabali wa usalama wao.
Hata hivyo RC Makonda amewahimiza wananchi kufuatilia tahadhari zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) pamoja na Vyombo vya Habari.


Comments
Post a Comment