BALOZI SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, PIA AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA KATIKA NCHI ZA MISRI NA ZAMBIA
Balozi wa China Nchini Tanzania Bibi Wang Ke alisema kukamilika kwa utanuzi wa ujenzi wa Eneo la Maegesho ya Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar utatoa fursa ya kuongezeka kwa huduma za usafiri wa anga baina ya Zanzibar na Mataifa mengine Duniani. Alisema matayarisho ya ujenzi huo katika hatua za awali za Awamu ya Pili aliyoyashuhudia baada ya kushuka kwenye Uwanja huo wa Ndege wa Zanzibar yamempa faraja yeye pamoja na Uongozi mzima wa Benki ya Kimataifa ya Exim ya Nchini China iliyoridhia kugharamia Mkopo wa ujenzi huo. Balozi Wang Ke alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo wa Kidiplomasia. Alisema Zanzibar inaweza kurejesha Heshima yake ya kuwa Kituo cha Kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma za Kibiashara kupitia mfumo wa kisasa wa Mawa...