MANISPAA ILALA YAVAMIA VIJIWE VYA MATEJA
Mkuu wa Idara ya Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu uhamasishaji na kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi. Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala na kikundi cha Joging wakielelea eneo la kufanya usafi Posta ya zamani. Msemaji wa Manispaa ya Ilala, Tabu shaibu alikiwajibika kufanya usafi wa mazingira. Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala na kikundi cha Joging wakifanya usafi Posta ya zamani eneo la ufukwe. Leonce Zimbandu MANISPAA Ilala imevamia vijiwe vya Mateja vilivyoko kwenye ufukwe wa Posta ya zamani kwa kufanya usafi wa Mazingira ikiwa ni utekekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli. Hatua hiyo imechukuliwa na Manispaa hiyo baada ya kubaini kuwa eneo hilo limekithiri kwa taka mchanganyiko, ikiwa viwembe, plastiki, makaratasi na mabaki ya vyakula. Mkuu wa Idara ya Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda aliyasema hayo alipokuwa akizung...